Ershadi: Iran ni mhanga mkubwa wa silaha za kemikali duniani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i74228-ershadi_iran_ni_mhanga_mkubwa_wa_silaha_za_kemikali_duniani
Naibu mwakilishi wa kudumu wa Iran katika umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mhanga mkubwa wa silaha za kemikali inatoa wito wa kutekelezwa kikamilifu, kwa njia athirifu na bila ya ubaguzi mkataba wa kuzuia silaha za kemikali.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 03, 2021 02:05 UTC
  • Zahra Ershadi
    Zahra Ershadi

Naibu mwakilishi wa kudumu wa Iran katika umoja wa Mataifa amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kama mhanga mkubwa wa silaha za kemikali inatoa wito wa kutekelezwa kikamilifu, kwa njia athirifu na bila ya ubaguzi mkataba wa kuzuia silaha za kemikali.

Zahra Ershadi amesema kuwa Iran itaendelea kutetea malengo ya mkataba wa kuzuia silaha za kemikali na inataka kutekelezwa kikamilifu na bila ya ubaguzi mkataba huo. Ershadi ameongeza kuwa, Iran inataka mkataba huo utekelezwe kote duniani na inaamini kuwa, ili kufikiwa lengo hilo muhimu utawala wa Israel unapaswa kulazimishwa kujiunga na mkataba huo haraka na bila ya masharti yoyote. 

Balozi wa Iran katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Iran ambayo ni mhanga mkubwa wa silaha za kemikali inalaani watumiaji na utumiaji wa silaha hizo popote na katika mazingira yote. 

Vilevile amepongeza juhudi zinazofanywa na serikali ya Syria katika kutekeleza mkataba huo na kusema kuwa: Kuharibiwa kikamilifu miradi ya silaha za kemikali ya Syria katika kipindi kifupi na katika mazingira ya kipekee ni kielelezo cha umuhimu wa hatua hiyo ya serikali ya Damascus.

Mkataba wa kuzuia silaha za kemikali ni miongoni mwa mikataba muhimu sana ya kimataifa inayopiga marufuku uzalishaji, urundikaji na utumiaji wa silaha za mauaji ya umati na silaha za kemikali. Mkataba huo ulipasishwa na nchi 165 wanachama wa Umoja wa Mataifa tarehe 13 Januari mwaka 1993 katika miji ya Paris na New York na ukaanza kutekelezwa tarehe 29 Aprili mwaka 1997.