Sep 04, 2021 08:00 UTC
  • Khatibzadeh: Viongozi wa sasa wa Marekani wanafuata njia iliyofeli ya serikali iliyopita

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema viongozi wa sasa wa Marekani wanafuata njia ileile iliyofeli na kugonga mwamba ya serikali iliyopita ya nchi hiyo.

Saeed Khatibzadeh ameyasema hayo kufuatia hatua ya serikali ya Marekani ya kuendeleza sera ya vikwazo dhidi ya Iran.

Kufuatia hatua ya wizara ya fedha ya Marekani ya kuyaweka majina ya raia wanne wa Kiirani kwenye orodha ya vikwazo ya nchi hiyo kwa kutegemea tuhuma bandia, msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema,  viongozi wa sasa wa Marekani wanafuata njia ileile iliyofeli na kugonga mwamba ya serikali iliyopita ya nchi hiyo.

Khatibzadeh ameongeza kuwa, waungaji mkono na madalali wa vikwazo ndani ya Marekani wameliona sanduku lao la wenzo wa vikwazo limebaki tupu kutokana na muqawama wa kiwango cha juu kabisa wa Iran; na kwa hiyo mara hii wanatumia sinario za ki hollywood ili kuweza kulifufua na kulipa uhai tena kwa kutumia anga ya vikwazo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameeleza bayana kwamba, Washington inapaswa itambue kuwa haina chaguo jengeine isipokuwa kuacha uraibu wake wa vikwazo na kutumia lugha na mwenendo wa heshima katika kuamiliana na Tehran.

Kwa kutegemea madai ambayo hayajathibitishwa, wizara ya fedha ya Marekani imeyaweka majina ya raia wanne wa Iran kwenye orodha yake ya vikwazo kwa madai ya kile eti ilichokiita "njama ya kutaka kumteka nyara mwanaharakati mmoja Muirani Mmarekani.../

Tags