-
Martin Griffiths : Upuuzaji wa Israel hauwezi kuendelea; ataka kulindwa raia
May 28, 2024 04:24Mratibu mkuu wa misaada na masuala ya dharura wa Umoja wa Mataifa amelaani mashambulizi ya utawala wa Israel katika kambi ya wakimbizi wa ndani wa Kipalestina katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza akisema kuwa upuuzaji wa Israel hauwezi kuendelea. Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ametaka kulindwa raia na kuruhusiwa kuelekea maeneo salama.
-
WHO: Dunia imetimiza nusu tu ya lengo la kimataifa la huduma muhimu za afya ifikapo 2025
May 28, 2024 04:15Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema licha ya hatua kubwa ya upashaji habari, ni watu milioni 585 tu ambao watafikiwa na huduma muhimu za afya ifikapo mwaka 2025.
-
Colombia yakata uhusiano na utawala wa Israel
May 28, 2024 03:01Waziri wa Mambo ya Nje wa Colombia ametangaza kukatwa uhusiano wa kidiplomasia wa nchi yake na utawala wa Kizayuni.
-
Watu 670 wapoteza maisha katika maporomoko ya udongo Papua New Guinea
May 27, 2024 02:26Maporomoko ya udongo huko kaskazini mwa Papua New Guinea yamepelekea watu wasiopungua 670 kupoteza maisha na kijiji kizima kuangamizwa.
-
US na UK zinaweza kushtakiwa kwa 'kushiriki' katika mauaji ya kimbari ikiwa amri ya ICJ itapuuzwa
May 26, 2024 22:50Mtaalamu wa Sheria wa Kituo cha Kimataifa cha Haki kwa Wapalestina (International Center of Justice for Palestinians, ICJP) amesema, uamuzi uliotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) wa kuuamuru utawala wa Kizayuni wa Israel usitishe uvamizi wake wa kijeshi dhidi ya mji wa Rafah ulioko kusini mwa Ukanda wa Ghaza ni hatua sahihi, lakini suala muhimu sasa hivi ni kuheshimiwa kwa kutekelezwa uamuzi huo.
-
Slovenia: Kulitambua taifa la Palestina ni wajibu wa kimaadili
May 26, 2024 22:49Waziri wa Mambo ya Nje wa Slovenia amesema kuitambua Palestina kama nchi huru ni jukumu la kimaadili.
-
Uamuzi wa Mahakama ya Hague kuhusu Rafah: Kushindwa kwingine kwa utawala wa Kizayuni
May 26, 2024 22:49Mahakama ya Kimataifa ya Haki iliyo na makao makuu yake mjini The Hague, Uholanzi , ambacho ni chombo cha juu zaidi cha mahakama cha Umoja wa Mataifa, iliamua Ijumaa, Mei 24, kwamba Israel lazima isimamishe "mara moja" mashambulizi yake ya kijeshi huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Maandamano ya kuitetea Palestina yashuhudiwa Ulaya licha ya vizingiti
May 26, 2024 09:48Miji na majiji makubwa ya Ulaya jana Jumamosi yalishuhudia maandamano ya kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza, sanjari na kutaka kusitishwa mara moja vita vya utawala wa Kizayuni dhidi ya eneo hilo lililozingirwa.
-
NATO yaituhumu China kuwa inachochea moto wa vita Ulaya kwa kuiunga mkono Russia
May 26, 2024 07:45Katibu Mkuu wa shirika la kijeshi la Magharibi NATO Jens Stoltenberg ameituhumu China kwamba inachochea vita barani Ulaya kwa kuiunga mkono Russia dhidi ya Ukraine.
-
Umoja wa Mataifa wakaribisha uamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Haki
May 26, 2024 06:35Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Masuala ya Dharura na Kibinadamu amekaribisha hukumu ya Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ inayoutawala utawala wa Kizayuni usimamishe mara moja operesheni za kijeshi katika mji wa Rafah Kusini mwa Gaza.