May 28, 2024 07:45 UTC
  • WHO: Dunia imetimiza nusu tu ya lengo la kimataifa la huduma muhimu za afya ifikapo 2025

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani amesema licha ya hatua kubwa ya upashaji habari, ni watu milioni 585 tu ambao watafikiwa na huduma muhimu za afya ifikapo mwaka 2025.

Tedros Adhanom Ghebreyesus ameuambia mkutano wa kila mwaka wa Baraza la Afya Duniani (WHA) kwamba watu bilioni 2 wanakabiliwa na matatizo ya gharama za ziada za malipo ya huduma za afya. 

Amesema nusu ya jamii ya watu duniani mwaka jana hawakupata huduma muhimu za afya akisema mwaka huo ulikuwa mwaka wa changamoto nyingi lakini pia walishuhudia mafanikio mengi. Amezitaja changamoto hizo kuwa ni pamoja na tetemeko la ardhi lililoikumba Uturuki na Syria, mapigano na hali ya machafuko huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Gaza, Haiti, Mynmar, Sudan na Ukraine.  

Tetemeko la ardhi nchini Syria 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO aidha amesema pengine tishio kubwa zaidi kwa afya wakati huu linatokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Amesema nchi 149 zimetia saini azimio la COP28 kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa na afya, na wafadhili waliahidi kutoa zaidi ya dola bilioni moja kushughulikia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa afya ya jamii.

 

Tags