-
Ukosoaji wa Amnesty International kwa njama za Marekani za kuficha jinai za Israel Gaza
Apr 26, 2024 23:05Agnes Callamard, Katibu Mkuu wa Shirika la Msamaha Duniani la Amnesty International, ameonya kuhusu kuendelea kwa ukiukaji wa haki za binadamu huko Gaza na kutangaza kuwa: Marekani inazuia kutuhumiwa Israel kwa kukiuka haki za binadamu katika Ukanda wa Gaza.
-
Bunge la EU ladhihirisha tena unafiki wa Magharibi kwa kulaani shambulio la kujibu mapigo la Iran dhidi ya Israel
Apr 26, 2024 07:37Bunge la Ulaya limedhihirisha tena sera za undumilakuwili za Magharibi kwa kupitisha azimio la kulaani shambulio la hivi karibuni la kujibu mapigo lililofanywa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kuzitolea wito nchi wanachama za umoja huo ziiwekee Tehran vikwazo vingine vipya na vikali zaidi.
-
Afisa wa nne wa Wizara ya Mambo ya Nje ya US ajiuzulu kupinga sera kuhusiana na vita vya Ghaza
Apr 26, 2024 07:28Msemaji wa kitengo cha Kiarabu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani amejiuzulu wadhifa wake kulalamikia na kupinga sera za serikali ya nchi hiyo katika vita vya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza.
-
Mtaalamu wa UN ataka Israel iwekewe vikwazo vya silaha, mafuta
Apr 26, 2024 04:35Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ardhi ya Palestina Inayokaliwa kwa Mabavu Francesca Albanese ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuweka vikwazo vya mafuta na silaha dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel unaoendeleza mauaji ya kimbari katika Ukanda wa Gaza.
-
Marekani yashadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani wa utawala wa Kizayuni na waungaji mkono wa Palestina
Apr 25, 2024 23:39Marekani ndiyo muungaji mkono mkubwa zaidi wa utawala wa Kizayuni wa Israel ambapo serikali ya Biden imetoa msaada mkubwa zaidi wa kijeshi na silaha kwa Tel Aviv wakati wa vita vya Gaza, ambavyo vimeingia katika mwezi wake wa saba.
-
Mamlaka za uchaguzi India zataka kupewa majibu kuhusu malalamiko dhidi ya Modi na Rahul Gandhi
Apr 25, 2024 23:37Mamlaka za uchaguzi India jana zilisema kuwa kuwa zinataka kupewa majibu kutoka chama tawala nchi hiyo cha Bharatiya Janata Party (BJP) na chama kikuu cha upinzani cha Indian National Congress juu ya madai ya ukiukaji wa sheria za uchaguzi katika hotuba zilizotolewa wakati wa kampeni za uchaguzi zinazoendelea kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo.
-
Wanachuo zaidi ya 100 wakamatwa California na Texas, US kwa kupinga vita vya Israel Ghaza
Apr 25, 2024 08:13Polisi nchini Marekani wamewakamata makumi ya wanachuo walioandamana katika Chuo Kikuu cha Texas huko Austin (UT Austin) na Chuo Kikuu cha Kusini mwa California (USC) huku maandamano yanayoongozwa na wanafunzi kupinga vita vya Israel dhidi ya Ghaza yakizidi kushika kasi nchini kote naye Spika wa Bunge Mike Johnson akipendekeza kuombwa msaada wa askari wa Gadi ya Taifa.
-
Rais wa Ureno asema inawapasa "walipe gharama" kwa waliyoyafanya enzi za ukoloni
Apr 25, 2024 06:41Rais wa Ureno amesema, nchi yake inabeba dhima ya jiinai na uhalifu iliofanya wakati wa biashara ya utumwa kupitia Bahari ya Atlantiki na enzi ya ukoloni, na kupendekeza kuwaa kuna haja ya kufidia hali hiyo.
-
Spika wa zamani wa Marekani: Netanyahu anapaswa ajiuzulu, amekwamisha amani kwa miaka kadhaa
Apr 25, 2024 06:31Spika wa zamani wa Baraza la Wawakilishi la Marekani Nancy Pelosi amesema, waziri mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel ni kizuizi cha kupatikana amani Ghaza na anapaswa ajiuzulu.
-
Amnesty International: Haki za binadamu duniani zingali zinakiukwa
Apr 25, 2024 04:00Shirika la Kimataifa la Msamaha Duniani la Amnesty International limetangaza kuwa, haki za binadamu zingali zinakabiliwa na tishio kubwa katika maeneo mbalimbali duniani.