Waislamu wa Kondoa Tanzania walaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu +VIDIO
Jul 30, 2023 04:42 UTC
Waislamu wa madhehebu ya Shia na Suni katika Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma nchini Tanzania kwa pamoja wamelaani vikali kuvunjiwa heshima kitabu kitakatifu cha Qur'ani.
Katika mkusanyiko wao wa pamoja, Waislamu hao wakiwa na mabango yaliyoandikwa: Ewe Dunia, Qur'ani yetu ni mstari mwekundu" wamesisitiza kwamba, katu hawakubaliani na kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani tukufu kitabu ambacho wameeleza kuwa ni katiba ya Waislamu.