Oct 06, 2023 03:27 UTC
  • UN: Mapigano Sudan yanasababisha kuongezeka kwa kasi mgogoro wa wakimbizi duniani

Mwakilishi Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Sudan amesema kuwa mapigano yanayoendelea nchini humo yanapelekea kuongezeka haraka mgogoro unapanuka wa wakimbizi duniani.

Clementine Nkweta Salami amesema kuwa, kwa wastani, zaidi ya watu 30,000 wanakimbia makazi yao nchini Sudan kila siku. Clentina Nkweta Salami ameongeza kuwa katika halia mbayo nusu ya wakazi wa Sudan wanahitaji misaada ya kibinadamu na ulinzi, mgogoro unaoikabili nchi hiyo pia umedumaza sekta ya afya nchini  huku asilimia 70 ya hospitali za Sudan zikiwa hazifanyi kazi. 

Clementine Nkweta Salami 

Mjumbe Mkazi wa Umoja wa Mataifa na Mratibu wa Masuala ya Kibinadamu huko Sudan ametahadharisha pia kuwa, mapigano yanayoendelea Sudan yanaweza kuathiri pakubwa usalama wa chakula nchini humo. 

Mapigano ya silaha yalianza huko Sudan Aprili 15 mwaka huu kati ya jeshi la nchi hiyo linaloongozwa na Jenerali Abdel Fattah al Burhan na Vikosi vya Usaidizi wa Haraka (RSF) chini ya uongozi wa Kamanda Hamdan Dagalo ambapo hadi sasa juhudi za upatanishi za kimataifa za kuhitimisha mapigano hayo na kuzishawishi pande hasimu kuketi kwenye meza ya mazungumzo zimegonga mwamba. 

 

Tags