Mgomo waendelea nchini Zimbabwe dhidi ya serikali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i11002-mgomo_waendelea_nchini_zimbabwe_dhidi_ya_serikali
Duru za habari nchini Zimbabwe zimeripoti kuendelea mgomo wa nchi nzima katika maeneo ya kazi, maduka na shule nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 10, 2016 22:13 UTC
  • Mgomo waendelea nchini Zimbabwe dhidi ya serikali

Duru za habari nchini Zimbabwe zimeripoti kuendelea mgomo wa nchi nzima katika maeneo ya kazi, maduka na shule nchini humo.

Rashweat Mukundu mchambuzi wa masuala ya kisiasa katika chuo cha utafiti cha 'Taasisi ya Kidemokrasia Zimbabwe' kilichopo Harare, mji mkuu wa nchi hiyo, amenukuliwa akisema kuwa, mgomo huo wa nchi nzima umesababisha hata idara za serikali na mahakama nyingi kuushiriki kutokana na kufeli siasa za serikali. Rashweat Mukundu ameongeza kuwa, hadi sasa wafanyakazi wa serikali wamejiunga pamoja na wapinzani katika mgomo. Mtafiti huyo amesisitiza kuwa, hasira zimeongezeka miongoni mwa raia wa Zimbabwe. Amesema kuwa, kuna uwezekano Zimbabwe ikatumbukia katika machafuko makubwa kutokana na kutoeleweka afya ya Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 92 na kuongezeka mivutano ndani ya chama tawala ya kuwania madaraka baada ya rais huyo.