Apr 23, 2024 08:01 UTC
  • Mbunge wa Kenya: Ulimwengu ‘umefurahishwa sana’ na operesheni ya Iran dhidi ya Israel

Mbunge mmoja wa bunge la Kenya amesema dunia nzima "imefurahishwa sana" na mashambulizi ya kulipiza kisasi ya Iran dhidi ya utawala haramu wa Israel kwani katika operesheni hiyo iliyopewa jina la 'Ahadi ya Kweli, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilikabiliana na satwa ya kibeberu ya Kizayuni na Magharibi.

Farah Maalim Mohamed, mbunge katika Bunge la Kitaifa la Kenya, amesema katika mahojiano na Press TV siku ya Jumatatu kwamba Iran iliuthibitishia ulimwengu kwamba "utawala wa kikoloni wa Marekani-Kizayuni-Magharibi" hauwezi tu kufanya wanavyotaka bila kuadhibiwa.

Maalim Mohamed amesema Iran ina uwezo wa kujilinda yenyewe na washirika wake na kusimama mbele ya adui wa Kizayuni na nchi za Magharibi ambazo zimezoea kuwaonea watu wengine duniani.

Mbunge huyo wa Kenya amesema: "Wanafikiri kwamba wanaweza kuua mtu yeyote wanayetaka kumuua, na kumpiga bomu mtu yeyote ambaye wanataka kumpiga bomu na hatuna haki ya kujibu mapigo."

"Nina furaha, nina furaha sana na nadhani ulimwengu wote una furaha isipokuwa utawala wa kichaa wa Magharibi ... Wao kwa mara ya kwanza wanaona kwamba sehemu ya dunia yenye ustaarabu wa zamani zaidi kuliko wao imesimama dhidi yao."

Maalim Mohamed amesisitiza kuwa ulimwengu hauwezi tena kuwatazama Wamagharibi na Wazayuni wakiwanyanyasa wengine kama ilivyo kuwa katika siku za nyuma. Amesema dhulma yoyote sasa itakabiliwa na jibu kutoka kwa wanaodhulumiwa.

Farah Maalim Mohamed amesema ulimwengu sasa unavutiwa na nchi kama Iran, Russia na China ambazo zinasema hazitakubali Wamaghribi na Wazayuni wavuke mipaka.

Mbunge huyo amesema, “Nadhani zaidi ya watu bilioni nane duniani wamefurahishwa sana na kile Iran ilichokifanya, na ninatumai nchi nyingi zaidi zitajiunga na Iran. Kila mtu ana furaha sana.”

Katika shambulio la pande kadhaa, lililopewa jina la Operesheni ya Ahadi ya Kweli, Iran ilivurumisha mamia ya ndege zisizo na rubani na makombora kuanzia Aprili 13 katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu zilizopachikwa jina la Israel ili kujibu hujuma za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya vituo jengo la ubalozi wa Iran katika mji mkuu wa Syria wa Damascus mnamo Aprili 1.