Kifo kimoja kati ya vitano vya ajali za barabarani duniani hutokea Afrika
(last modified Thu, 18 Jul 2024 02:29:44 GMT )
Jul 18, 2024 02:29 UTC
  • Kifo kimoja kati ya vitano vya ajali za barabarani duniani hutokea Afrika

Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema katika ripoti yake kuwa ajali ya barabarani katika muongo uliopita zimeongezeka kwa kiasi kikubwa katika kanda ya Afrika, na kwamba mwaka 2021 pekee karibu watu 250,000 walipoteza maisha katika ajali za barabarani barani humo.

Ripoti ya  WHO kuhusu Usalama Barabarani mwaka 2023 kwa Kanda ya Afrika imeeleza kuwa bara la Afrika linachangia karibu moja ya tano ya vifo vyote vya barabarani ulimwenguni, licha ya bara hilo kuwa na asilimia 15 ya idadi ya watu duniani.

Matokeo ya ripoti hii yanaashiria wasiwasi mkubwa wa afya ya umma kwa nchi za Kiafrika, huku mamia ya maelfu ya watu wakipoteza maisha katika ajali ambazo zingeweza kuzuiwa. 

Sisi kama WHO tumejipanga kushirikiana na nchi mbalimbali kuzuia tishio hilo linaloweza kuzuilika na kuendelea kuuunga mkono kikamilifu juhudi zote ili kuzifanya barabara zetu salama kwa  waendeshamagari na watembea kwa miguu ,” amesema Dr. Matshidiso Moeti, Mkurugenzi wa WHO kanda ya Afrika. 

Dr. Matshidiso Moeti