Watoto waandamana Nigeria kuwaunga mkono watoto wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i116090-watoto_waandamana_nigeria_kuwaunga_mkono_watoto_wa_gaza
Watoto wa Nigeria wamekusanyika katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Bauchi na kupiga nara za kuwaunga mkono watoto wa Kipalestina, hasa wale wanaoishi katika Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-09-06T23:20:04+00:00 )
Sep 06, 2024 23:20 UTC
  • Watoto waandamana Nigeria kuwaunga mkono watoto wa Gaza

Watoto wa Nigeria wamekusanyika katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Bauchi na kupiga nara za kuwaunga mkono watoto wa Kipalestina, hasa wale wanaoishi katika Ukanda wa Gaza.

Watoto hao wa Kinigeria wamelaani jinai za utawala haramu wa Israel huko Gaza hasa dhidi ya watoto wadogo wasio na hatia yoyote na kutoa mwito wa kuchukuliwa hatua za kuwalinda watoto wa Ukanda huo.

Katika mahojiano maalumi na Shirika la Habari la Iran Press, Sabira Musa Bayi Muhammad msichana wa umri wa miaka minane  amesema, "Mwezi mtukufu wa Rabi ul Awwal unapoanza, huambatana na sherehe na furaha ambapo Mtume wetu kipenzi alizaliwa ndani yake, lakini kwa sasa hatuwezi kuwasahau kaka na dada zetu katika Gaza hasa watoto ambao wanaptia kipindi kigumu kutokana na hujuma na mashambulio ya kinyama ya Israel dhidi ya makazi yao..

Zainab Habib, mwanafunzi mwingine aliyeshiriki katika maandamano hayo amezungumza na Iran Press kuhusu umuhimu wa maandamano hayo na kusema:

 

Tunawalilia. Wazazi wao wanauawa na jeshi la kigaidi la Israel. Hawana chakula. Kwa hakika mioyo yetu iko pamoja nao na tunawakumbuka daima. Mwenyezi Mungu awapunguzie mateso na kuwaangamiza magaidi wa Israel.

Wakati huo huo, Mfuko wa Kuhudumia Watoto (UNICEF) umetangaza kwamba Gaza, iliyoharibiwa na vita vya miezi 11 vya Israel, "tayari ni mahali hatari zaidi duniani kuwa mtoto, na licha ya kusitishwa mashambulizi ya Israel kwa ajili ya chanjo ya polio, kampeni ya kutoa chanjo inakabiliwa na hatari kubwa na vikwazo visivyoweza kufikirika, ikiwa ni pamoja na barabara zilizoharibika na kubomolewa miundombinu ya afya, watu waliokimbia makazi yao, uporaji na kuvurugwa njia za usambazaji.