Ramaphosa: Afrika Kusini kutoa kipaumbele kwa mahitaji na matarajio ya Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i116972-ramaphosa_afrika_kusini_kutoa_kipaumbele_kwa_mahitaji_na_matarajio_ya_afrika
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa nchi yake itakapochukua uwenyekiti wa kundi la G-20 baadaye mwaka huu, nchi hiyo itatoa kipaumbelea kwa mahitaji nan matarajio ya Afrika na Ulimwengu wa Kusini.
(last modified 2024-10-01T02:51:27+00:00 )
Oct 01, 2024 02:51 UTC
  • Ramaphosa: Afrika Kusini kutoa kipaumbele kwa mahitaji na matarajio ya Afrika

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini amesema kuwa nchi yake itakapochukua uwenyekiti wa kundi la G-20 baadaye mwaka huu, nchi hiyo itatoa kipaumbelea kwa mahitaji nan matarajio ya Afrika na Ulimwengu wa Kusini.

"Kama pande iliyotia saini Mkataba wa Baadaye( Pact for the Future) tunataka maendeleo endelevu yanayoendeshwa na watu yawe uhakika wa mambo", amesema Rais wa Afrika Kusini.

Mkataba kwa jina "Pact for the Future" unazitaka nchi wanachama kuimarisha hatua za kimataifa kuelekea ajenda mpya ya amani.

Rais Cyril Ramaphosa  pia ameashiria msimamo wa nchi yake katika Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uliofanyika wiki iliyopita mjini New York Marekani ambako alibainisha kwa mara nyingne tena kuwa maendeleo endelevu yanaweza kupatikana tu pale chini ya usimamizi na uendeshaji wa taasisi shirikishi, tendaji na zenye kasi za kimataifa.

Alisema, hii ina maana kuwa taasisi kama Umoja wa Mataifa na taasisi za kifedha kama IMF zinahitaji kufanyiwa marekebisho ya kimsingi. 

Rais wa Afrika Kusinii ametoa mfano mlipuko wa ugonjwa wa Uviko-19 ambao amesema uliweka wazi mapungufu makubwa ya mfumo wa fedha wa kimataifa.

Janga la corona lilivyoitatiza dunia 

Amesema, nchi za kipato cha chini  zilihangaika kupata misaada ya kifedha na mingineyo kutoka kwa taasisi za kimataifa ili kusaidia serikali zao  kukabiliana na janga la corona."