UN: Wahamiaji wa Kiafrika na wakimbizi wanaendelea kutafuta njia za kuelekea Ulaya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i116984-un_wahamiaji_wa_kiafrika_na_wakimbizi_wanaendelea_kutafuta_njia_za_kuelekea_ulaya
Umoja wa Mataifa umesema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, umesajili zaidi ya wakimbizi 350,000 wa Sudan na watu wanaotafuta hifadhi maeneo ya Afrika Kaskazini, huku wahamiaji 97,000 wakiiingia Libya tangu mwezi Aprili mwaka jana.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 01, 2024 10:14 UTC
  • UN:  Wahamiaji wa Kiafrika na wakimbizi wanaendelea kutafuta njia za kuelekea Ulaya

Umoja wa Mataifa umesema kuwa, tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, umesajili zaidi ya wakimbizi 350,000 wa Sudan na watu wanaotafuta hifadhi maeneo ya Afrika Kaskazini, huku wahamiaji 97,000 wakiiingia Libya tangu mwezi Aprili mwaka jana.

Ni muhimu kutilia maanani kuwa changamoto hizo za uhamiaji  hazianzii Afrika Kaskazini. Hivyo kunahitajika kufanyika uchunguzi wa haraka wa chanzo cha changamoto hizo kuanzia mizizi ya safari. Hayo yamesemwa na Sivanka Dhanapala, Mkurugenzi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR).

Vile vile,  Sivanka Dhanapala amesema kuwa, kati ya mwezi  Januari na Agosti mwaka huu, inakadiriwa kwamba zaidi ya wakimbizi na wahamiaji 134,000 waliondoka kwa usafiri wa baharini kutoka kaskazini na magharibi mwa Afrika kuelekea barani Ulaya. Idadi hiyo imepungua kidogo ikilinganishwa na idadi ya mwaka jana ya wakimbizi na wahamiaji hao. 

Wahamiaji wa Kiafrika na wakimbizi wanaendelea kutafuta njia za kuelekea Ulaya

Kwa upande wake, Par Liljert, Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji amewasilisha ripoti fupi kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akisema kwamba, mambo ambayo yanawafanya watu kuacha nyumba zao na makazi yao na kujiingiza kwenye changamoto kali wanazopambana nazo wakiwa njiani kujaribu kuhamia maeneo mengine ni changamoto nzito hivi sasa ambazo zinahitaji kuchukuliwa hatua thabiti na za haraka za kukabiliana nazo.