Guterres: Hatua madhubuti zichukuliwe kushughulikia migogoro na umaskini Afrika
(last modified Tue, 22 Oct 2024 15:15:49 GMT )
Oct 22, 2024 15:15 UTC
  • Antonio Guterres
    Antonio Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa hatua madhubuti zinapasa kuchukuliwa ili kushughulikia mabadiliko ya tabianchi, migogoro na umaskini barani Afrika.

Antonio Guterres amesema kuwa Afrika ni bara la matumaini lakini linakabiliwa na changamoto ambazo zimekita mizizi katika historia na zimechochewa na mabadiliko ya hali ya tabianchi, migogoro mbalimbali na umaskini. 

Amesema kuwa wanawake wa Kiafrika mara nyingi "hubeba mzigo mkubwa wa matatizo haya na kusisitiza kuwa masuala haya yanahitaji "hatua madhubuti na mshikamano mpya."

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameongeza kuwa taasisi za kimataifa ziliasisiwa wakati sehemu kubwa ya bara la Afrika ilipokuwa chini ya utawala wa kikoloni na aghalabu ya taasisi hizi zimeshindwa kukidhi mataraji na haki za watu wa Afrika.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, hadi sasa bara la Afrika halina mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la umoja huo na amezikosoa taasisi za kimataifa za fedha kuwa mara nyingi zimeshindwa kukidhi mahitaji ya nchi za Kiafrika ama iwe ni kuhusiana na madeni yanayozikabili au kuhusu athari za mabadiliko ya tabianchi  ambayo hayakusababishwa na nchi hizo. 

Guterres: Bara la Afrika linapasa kuwa na mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la UN 

 

Tags