Nchi zilizoathiriwa zaidi Afrika zapokea dozi laki nane za chanjo ya MPOX
Shirika la Afya Duniani (WHO) imetenga dozi 899,000 za chanjo ya MPOX kwa nchi tisa za Afrika ambazo zimeathiriwa zaidi na mlipuko wa sasa wa ugonjwa huo.
Kwa mujibu wa taarifa, dozi hizo tayari zimewasili katika nchi 9 barani Afrika ambazo zimeathiriwa sana na ugonjwa wa MPOX ambao uko barani humo hivi sasa.
WHO ilitangaza mpox ni dharura ya afya ya umma duniani kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka miwili hapo mwezi Agosti, baada ya aina mpya ya virusi vinavyoitwa Clade Ib, kusambaa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwenda nchi jirani.
Mwaka huu pekee, ugonjwa huo umesababisha vifo zaidi ya 1,000 katika bara zima la Afrika, ambapo zaidi ya kesi 46,000 zikiripotiwa DRC, na kwa msingi hiyo nchi hiyo itapata asilimia 85 ya dozi zilizotengwa za chanjo. Asilimia 15% iliyobaki ya chanjo itatumika Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast, Kenya, Liberia, Nigeria, Rwanda, Afrika Kusini na Uganda.
MPOX ni ugonjwa wa virusi unaopatikana kwa Wanyama (hasa Nyani), kutokana na shughuli za kibinadamu ugonjwa huo umetoka kwa Wanyama na kuhamia kwa binadamu na kupelekea kuambukizana binadamu kwa binadamu.
Dalili za MPOX hazitofautiani sana na zile za malaria yani Mwili kuwa na joto kali (kuchemka) ,mafua, mwili kuuma au kuuma na kukereketa kwa koo na pia kutokwa na mtoki kwenye shingo au pembezoni mwa mapaja na kwenye makwapa.