DRC yaanzisha uchunguzi baada ya ugonjwa usiojulikana kuua watu 79
Takriban watu 79 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa ajabuusiojulikana katika jimbo la kusini magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi uliopita, huku waziri wa afya akitangaza kwamba timu ya wataalam imetumwa ili kubaini asili halisi ya ugonjwa huo.
Hali katika kijiji cha Panzi katika jimbo la Kwango ni ya kutisha ,baada ya watu 60 kupoteza maisha baada ya kupata uongojwa huo usiojulikana kati ya Novemba 10 na 25, na kufanya jumla ya vifo katika mkoa huo kufikia 79 mwezi uliopita.
Waziri wa Afya Samuel Kamba Roger alisema katika taarifa iliyotolewa Jumatano kwamba dalili za ugonjwa huo zinaweza kuashiria magonjwa kadhaa ya kuambukiza, ikiwa ni pamoja na mpox na Ebola, ambayo yote yamesababisha wasiwasi mkubwa nchini DR Congo.
Aliongeza kuwa serikali imetuma timu ya wataalam wa magonjwa ya milipuko ili kutathmini hali na kujua asili ya ugonjwa huo.
Amethibitisha kuwa mlipuko huu tayari umesababisha vifo vya watu 79, jambo ambalo limeitia hofu serikali ya mkoa wa Kwango.
DRC ina historia ndefu ya kupambana na magonjwa ya mlipuko, na serikali hufuatilia kwa karibu masuala ya magonjwa ili kukabilin macho kukabiliana na magonjwa hayo.. Juhudi za afya ya umma, ikiwa ni pamoja na ufuatiliaji wa magonjwa na uhamasishaji wa jamii, ni muhimu kudhibiti hali hii na kuzuia kuenea kwa magonjwa ya kuambukiza.
Mpox, ingawa ni hatari kidogo kuliko virusi vya Ebola, imeibuka tena katika baadhi ya maeneo ya Afrika, na kuzua wasiwasi kuhusu maambukizi yake.
Kwa upande mwingine, Ebola, inayojulikana kwa kiwango cha juu cha vifo na maambukizi ya haraka, bado ni tishio linaloendelea nchini DR Congo, huku milipuko ya mara kwa mara ikiathiri jamii zilizo hatarini.