Iran yaishukuru Burkina Faso kwa kupinga azimio la IAEA dhidi ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i119730-iran_yaishukuru_burkina_faso_kwa_kupinga_azimio_la_iaea_dhidi_ya_iran
Balozi wa Iran amekutana na  Waziri wa Usalama wa Burkina Faso, Mahamadou Sana, ambapo wamejadili masuala ya uhusiano wa pande mbili na matukio ya kimataifa.
(last modified 2024-12-05T04:16:25+00:00 )
Dec 05, 2024 04:16 UTC
  • Iran yaishukuru Burkina Faso kwa kupinga azimio la IAEA dhidi ya Iran

Balozi wa Iran amekutana na  Waziri wa Usalama wa Burkina Faso, Mahamadou Sana, ambapo wamejadili masuala ya uhusiano wa pande mbili na matukio ya kimataifa.

Katika kikao hicho cha Jumatano, Balozi Mojtaba Faghihi aliwasilisha shukurani za dhati za Iran kwa serikali ya Burkina Faso kwa kuiunga mkono Iran katika kikao cha   Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA).

Mnamo tarehe 21 Novemba, shirika hilo la kimataifa lilipitisha azimio jipya dhidi ya mpango wa nyuklia wa Iran wenye malengo ya amani , ambapo nchi 19 kati ya 35 ziliidhinisha azimio hilo. Burkina Faso ilikuwa mojawapo ya nchi tatu zilizopinga azimio lililokuwa dhidi ya Iran.

Msimamo wa Burkina Faso unaonyesha nguvu na uhuru wake katika ngazi ya kimataifa.

Katika kikao hicho, Balozi Faghihi amesisitiza kuhusu  "uungaji mkono usioyumba" wa Iran kwa Burkina Faso katika vita vyake dhidi ya ugaidi. Ameongeza kuwa Iran iko tayari kuipa Burkina Faso ujuzi ilionao ili kusaidia kurejesha amani na usalama nchini humo.

Tangu kuingia madarakani serikali ya kijeshi inaoungwa mkono na wananchi wa Burkina Faso, Iran na Burkina Faso zimekuwa zikiimarisha uhusiano wao.