Uchaguzi wa Rais na Bunge Ghana unafanyika leo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i119806-uchaguzi_wa_rais_na_bunge_ghana_unafanyika_leo
Mamilioni ya wananchi wa Ghana leo Jumamosi wanaelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kumchagua rais mpya na wawakilishi wa bunge huku nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika inayojulikana kwa akiba kubwa ya dhahabu na uzalishaji wa kakao ikiwa katika hali ngumu ya kiuchumi.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Dec 06, 2024 22:56 UTC
  • Uchaguzi wa Rais na Bunge Ghana unafanyika leo

Mamilioni ya wananchi wa Ghana leo Jumamosi wanaelekea kwenye masanduku ya kupigia kura kumchagua rais mpya na wawakilishi wa bunge huku nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika inayojulikana kwa akiba kubwa ya dhahabu na uzalishaji wa kakao ikiwa katika hali ngumu ya kiuchumi.

Weledi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa uchaguzi wa leo unaweza kuleta mabadiliko au ukaendelea kuwa ni mwendelezo hali iliozeleka nchini Ghana.  

Rais Nana Akufo-Addo hagombei katika uchaguzi huu. Mahamudu Bawumia Makamu wa Rais wa Ghana anayekiwalisha chama tawala cha NPP anachuana na kiongozi wa chama cha upinzan NDC, John Dramani Mahama, ambaye aliwahi kuwa rais wa Ghana. 

Hata hivyo, uchaguzi wa rais wa leo nchini Ghana unaweza kuvuruga udhibiti wa jadi wa vyama hivyo viwili licha ya kuwepo wagombea 13 katika uchaguzi wa leo wakiwemo watu mashuhuri kama Alan Kyerematen, waziri wa zamani, na mfanyabiashara mtajika, Nana Kwame Bediako.

Jitihada za Mahamudu Bawumia za kutaka kuwa Muislamu wa kwanza kuiongoza Ghana; nchi ambayo ina idadi kubwa zaidi ya Wakristo, zinaongeza vuguvugu na kuzidisha joto la kipekee kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa kesho. 

Mahamudu Bawumia

Wananchi wa Ghana wasiopungua milioni 18.7 waliojiandikisha kupiga kura leo Jumamosi watamchagua rais mpya na wawakilishi wa bunge 276.

Vituo vya kupigia kura vitakuwa wazi kuanzia saa moja asubuhi na kufungwa saa kumi na moja jioni kwa wakati wa Ghana.

Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo imesema kuwa matokeo ya uchaguzi wa bunge yatatangazwa siku ya Jumatatu na kufuatiwa na ya urais siku moja baadaye.