Kiongozi wa Burkina Faso amteua waziri mkuu mpya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i119884-kiongozi_wa_burkina_faso_amteua_waziri_mkuu_mpya
Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa Burkina Faso na kuchukua nafasi ya Apollinaire Joachim Kyelem de Tambela, ambaye alifutwa kazi Ijumaa na Rais Kapteni Ibrahim Traore.
(last modified 2024-12-08T10:47:08+00:00 )
Dec 08, 2024 10:47 UTC
  • Kiongozi wa Burkina Faso amteua waziri mkuu mpya

Rimtalba Jean Emmanuel Ouedraogo ameteuliwa kuwa waziri mkuu wa Burkina Faso na kuchukua nafasi ya Apollinaire Joachim Kyelem de Tambela, ambaye alifutwa kazi Ijumaa na Rais Kapteni Ibrahim Traore.

Matias Traore, Katibu Mkuu wa Baraza la Mawaziri, ambaye aliwasilisha agizo hilo, amesema, "Atawajibika, katika siku zijazo, kuunda serikali kwa mwendelezo wa hatua za serikali, kushughulikia mambo yaliyokuwa yakishughulikiwa na serikali iliyovunjwa.”

Ouedraogo, ambaye ni mwandishi wa habari hapo awali aliwahi kuwa waziri wa serikali anayehusika na mawasiliano.

Hakuna sababu iliyotolewa ya kufutwa kazi na kuvunjwa serikali iliyokuwepo hapo hapo awali.

Katika nchi jirani ya Mali, Rais Jenerali Assimi Goita alimfuta kazi Waziri Mkuu Choguel Kokalla Maiga tarehe 11 Novemba, siku chache baada ya Maiga kuchukua hatua nadra ya kuwakosoa watawala wa kijeshi.

Burkina Faso, Mali na Niger ziliunda Muungano wa Nchi za Sahel mwezi Septemba 2023 na kutangaza kuundwa kikosi cha pamoja cha kijeshi ili kukabiliana na changamoto za usalama zinazosababishwa na makundi ya kigaidi katika nchi zao.