Zaidi ya watu 100 wauawa katika mashambulizi ya anga Khartoum
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i119984-zaidi_ya_watu_100_wauawa_katika_mashambulizi_ya_anga_khartoum
Zaidi ya watu mia moja wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi katika mji mkuu wa Sudan Khartoum na eneo la magharibi la Darfur.
(last modified 2024-12-10T23:17:14+00:00 )
Dec 10, 2024 23:17 UTC
  • Zaidi ya watu 100 wauawa katika mashambulizi ya anga Khartoum

Zaidi ya watu mia moja wameripotiwa kuuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi katika mji mkuu wa Sudan Khartoum na eneo la magharibi la Darfur.

Duru nyingi zimeripoti madai ya vifo vingi huku jeshi likizidisha mashambulizi ya anga katika maeneo yanayodhibitiwa na Kikosi cha Usaidizi wa Haraka (RSF).

Mashirika ya haki za binadamu na kisiasa nchini Sudan yamelaani mashambulizi ya anga ya jeshi la nchi hiyo, na kuyataja kuwa mauaji ya kutisha.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanalishutumu jeshi, ambalo limekuwa likipigana dhidi ya kundi la wanamgambo, RSF, tangu Aprili mwaka jana, kwa kusababisha vifo vya raia.

Jeshi pia linatuhumiwa kushambulia soko na hospitali zenye shughuli nyingi huko Darfur, eneo ambalo kwa kiasi kikubwa linadhibitiwa na vikosi vya RSF.

Hata hivyo jeshi la Sudan limekanusha kuwalenga raia, lakini pande zote mbili zimeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita.

Mapigano yameongezeka katika maeneo tofauti ya Sudan katika wiki za hivi karibuni huku jeshi likijitahidi kurejesha eneo ambalo limepoteza kwa RSF.

Mapigano kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF yalianza tangu Aprili mwaka jana; na hadi sasa watu zaidi ya elfu ishirini wameuawa na wengine wasiopungua milioni kumi wamekuwa wakimbizi.