Amnesty International: Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametenda uhalifu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120008-amnesty_international_wanajeshi_wa_jamhuri_ya_kidemokrasia_ya_congo_wametenda_uhalifu
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetoa taarifa na kuwatuhumu maafisa wakuu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwamba, wamehusika na vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu.
(last modified 2024-12-11T07:22:58+00:00 )
Dec 11, 2024 07:22 UTC
  • Amnesty International: Wanajeshi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wametenda uhalifu

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limetoa taarifa na kuwatuhumu maafisa wakuu wa jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwamba, wamehusika na vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Kwa mujibu wa Amnesty International, wanajeshi hao wanatuhumiwa uhalifu kwa huo kufuatia mauaji ya mwaka jana katika mji wa kaskazini mashariki wa Goma ambapo watu 56 waliuawa. Maafisa waliotajwa katika ripoti hiyo iliyotolewa siku ya Jumatano ni Constant Ndima Kongba, aliyekuwa gavana wa kijeshi wa jimbo la Kivu Kaskazini, maafisa wa jeshi Kanali Mike Mikombe Kalamba na Meja Peter Kabwe Ngandu.

Kulingana na shirika lisilo la kiserikali, "vikosi vya usalama vya Kongo vilijihusisha na mauaji" kwa kuwafyatulia risasi waandamanaji mnamo Agosti 30, 2023 huko Goma, makao makuu ya mkoa wa Kivu Kaskazini (mashariki), eneo linalokabiliwa na ghasia za makundi yenye silaha kwa zaidi ya miaka 30.

"Takriban watu 56 waliuawa kinyume cha sheria na zaidi ya 80 kujeruhiwa," Amnesty inasema. Wengi wa wahanga walikuwa wa vuguvugu la kidini-fumbo, Imani ya Kiyahudi na Masihi kuelekea Mataifa (FNJMN), ambayo kiongozi wake aliitisha maandamano dhidi ya Kikosi cha Kusimamia Amani cha Umoja wa Mataifa nchini DRC (MINUSCO).