DRC yabadili msimamo kuhusu kuondoka kikosi cha MONUSCO
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i120200-drc_yabadili_msimamo_kuhusu_kuondoka_kikosi_cha_monusco
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebadilisha msimamo wake kuhusu mchakato wa kuondooka nchini humo kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO).
(last modified 2024-12-15T23:12:40+00:00 )
Dec 15, 2024 23:12 UTC
  • DRC yabadili msimamo kuhusu kuondoka kikosi cha MONUSCO

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebadilisha msimamo wake kuhusu mchakato wa kuondooka nchini humo kikosi cha kusimamia amani cha Umoja wa Mataifa (MONUSCO).

Wakati uhuishaji wa mamlaka ya MONUSCO, uliopangwa kufanyika Desemba 19, unakaribia, serikali ya DRC imebadili mtazamo wake. Wakati mwaka jana serikalii ya Kinshasa ilitaka MONUSCO kuondoka haraka kwenye ardhi yake, sasa inachagua ujumbe huu kuondoka hatua kwa hatua na kwa mfumo ulioratibiwa.

Mpango wa awali wa kuodoka kwa wanajeshi wa MONUSCO uligawanywa katika awamu tatu: Kivu Kusini, Kivu Kaskazini na Ituri. Ingawa serikali inadai kuwa imekamilisha kwa mafanikio awamu ya kwanza katika mkoa wa Kivu Kusini, hali halisi kweye katika mkoa huo bado ni ngumu. Kwa mfano, urejeshaji wa kambi ya Kamanyola mwezi Februari ulionekana kuwa mgumu. Maafisa wa polisi wa Kongo waliotumwa katika uwanda wa Ruzizi, wakichukua nafasi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, wanakosa vifaa na ni wadogo, mbali na uwezo wa MONUSCO.

Kinshasa ambayo inakabiliwa na changamoto hizi, kwa hivyo inapendekeza uondoaji unaotanguliwa na tathmini makini. Mamlaka pia inataka uhamisho wa taratibu wa kazi muhimu, kama vile ulinzi wa raia, kwa msaada wa moja kwa moja wa wataalam na rasilimali za MONUSCO.