Ugonjwa 'usiojulikana' waua makumi ya watu DRC; mapigano yanaendelea
Ugonjwa usiojulikana umeua watu zaidi ya 50 katika eneo la Bansakusu, jimbo la Equateur, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Takriban watu 2,000 wamekimbia Bomate, yapata kilomita 25 (zaidi ya maili 15) kutoka Basankusu, kitovu cha mripuko huo, vyombo vya habari vimenukuu taarifa ya Seneta Jean-Paul Boketsu Bofili wa jimbo la Equateur.
Kwa mujibu wa Bofili, dalili za ugonjwa huo ambao haujatambuliwa kufikia sasa ni pamoja na homa ya hemorrhagic, maumivu ya kichwa, kuumwa na viungo na sehemu ya chini ya mgongo.
"Kufikia sasa, kumekuwa na vifo zaidi ya 36 vilivyoripotiwa na eneo la Basankusu katika wiki moja, yaani, kipindi cha kuanzia Februari 3 hadi 9, na zaidi ya vifo 50 tangu kuzuka kwa ugonjwa huo wiki chache nyuma katika eneo hili, ambalo lina wakaazi wapatao 5,000," seneta huyo amesema.

Katika hatua nyingine, idadai ya raia waliouawa katika shambulio la usiku lililofanywa na kundi lenye silaha la CODECO kwenye makundi ya vijiji mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imeongeze na kufikia 80,
Hayo yamesemwa na Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Kongo, MONUSCO na kueleza kuwa, idadi hiyo mpya ya vifo inazidi kwa mbali makadirio ya awali ya takriban watu 51 waliouawa, ambayo mamlaka za mitaa zilitangaza mara baada ya shambulio lililotokea usiku wa kuamkia Jumatatu katika eneo la Djugu, jimbo la Ituri.