Benin yarejesha kiti cha kifalme kilichoporwa na wazungu wakati wa utawala wa kikoloni
Wizara ya Utalii, Utamaduni na Sanaa ya Benin imetangaza kwamba kitu cha nadra cha kifalme kinachoitwa "Katakli" kitarejeshwa rasmi nchini humo kutoka Finland, ikiwa ni hatua ya hivi karibuni zaidi katika juhudi zinazoendelea kufanywa na Benin kurejesha urithi wake wa kitamaduni ulioporwa na wakoloni wa Ulaya.
"Kataklé", kiti cha kifalme chenye miguu mitatu, kilitumika kitamaduni wakati wa sherehe za kutawazwa katika ufalme wa kihistoria wa Dahomey, ambao leo upo ndani ya mipaka ya Benin.
Kiti hicho ambacho ni nembo ya nguvu, umoja, na utulivu kiliporwa mara ya kwanza na vikosi vya wakoloni wa Ufaransa mnamo 1892, kabla ya kuishia kwenye Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Finland mnamo 1939.
Hafla rasmi ya makabidhiano imepangwa kufanyika katika mji mkuu wa kiuchumi wa Benin, Cotonou.
Katika taarifa iliyotolewa Novemba mwaka jana, Jumba la Makumbusho la Kitaifa la Finnish lilieleza kwamba "umuhimu wa Katakli huko Dahomey au historia yake kama kitu kilichoporwa haukujulikana nchini Ufini," na kuongeza kwamba "kurejeshwa kwa Kataklé nchini Benin kunakamilisha urejeshaji wa mali muhimu za kitamaduni na za kihistoria, baada ya kurudishwa viapande 26 vya kihistoria kutoka Ufaransa mwakak 2021."