Rwanda yajiondoa katika muungano wa Afrika ya Kati ikitoa lawama kwa DRC
(last modified Sun, 08 Jun 2025 12:31:49 GMT )
Jun 08, 2025 12:31 UTC
  • Rwanda yajiondoa katika muungano wa Afrika ya Kati ikitoa lawama kwa DRC

Rwanda imetangaza kujiondoa katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika ya Kati (ECCAS), ikimshutumu nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa "kutumia njama kushawishi nadharia ya" umoja huo.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Rwanda imesema katika taarifa yake kwamba, “haki ya Rwanda ya urais wa zamu, kama ilivyoainishwa katika Kifungu cha 6 cha mkataba [kuanzisha ECCAS], ilipuuzwa kwa makusudi" kwa maagizo kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ilitaja kutengwa kwa Rwanda katika mkutano wa 22 wa kawaida wa ECCAS huko Kinshasa mwaka 2023 chini ya uenyekiti wa Congo huku mvutano kati ya nchi hizo mbili ukipamba moto.

Serikali ya Rwanda ilibainisha kuwa, hali hiyo ni kielelezo kipya cha “ziada” za shirika hilo na haioni sababu tena ya kuendelea kuwa mwanachama wa shirika ambalo utendaji wake unaenda kinyume na kanuni na manufaa yake.

Uteuzi wa mwenyekiti mpya wa ECCAS, uliopangwa kufanyika siku ya Jumamosi, uliahirishwa baada ya DRC kuripotiwa kupinga uhamisho wa mwenyekiti wa zamu kutoka Guinea ya Ikweta na kupewa Rwanda.

Hatua hiyo muhimu ya Kigali iliyotangazwa mwishoni mwa mkutano wa 26 wa kawaida huko Malabo, Equatorial Guinea, inaashiria mvutano unaoongezeka kati ya Rwanda na Congo kuhusu mzozo wa mashariki mwa Congo.

Ripoti zilisema kuwa, juhudi za mamlaka za awali za kujaribu kupunguza mvutano kati ya Kinshasa na Kigali katika mikutano ya faragha kando ya mkutano huo zilishindwa.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inaishutumu Rwanda kwa kuwaunga mkono waasi wa M23 wanaopigana mashariki mwa DRC jambo ambalo Kigali inakanusha.