Waziri wa Mambo ya Nje: Uganda haijakubaliana na Marekani kupokea wahamiaji haramu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i129766-waziri_wa_mambo_ya_nje_uganda_haijakubaliana_na_marekani_kupokea_wahamiaji_haramu
Uganda imesema kuwa haijafikia makubaliano na Marekani kuwapokea nchini humo wahamiaji haramu kwa sababu haina miundomsingi inayohitajika kufanya hivyo.
(last modified 2025-08-20T11:57:53+00:00 )
Aug 20, 2025 11:57 UTC
  • Waziri wa Mambo ya Nje: Uganda haijakubaliana na Marekani kupokea wahamiaji haramu

Uganda imesema kuwa haijafikia makubaliano na Marekani kuwapokea nchini humo wahamiaji haramu kwa sababu haina miundomsingi inayohitajika kufanya hivyo.

Okello Oryem Waziri wa Mambo ya Nje wa Uganda ameeleza kuwa, ninavyofahamu mimi hakuna makubaliano tuliyofikia na Marekani. " Hatuna suhula na miundomsingi ya kuwezesha kuwapokea nchini wahamiaji haramu kama hao."

Siku ya Jumanne shirika lal habari la CBS lilinukuu nyaraka za ndani na kuripoti kuwa Washington imefikia makubaliano na Honduras na Uganda ya kuwapokea katika nchi hizo wahamiaji haramu kama sehemu ya juhudi za kufikia mikataba mingine zaidi na nchi mbalimbali ambazo zitakubali kuwapokea wahamiaji haramu kutoka Marekani ambao si raia wa nchi hizo. 

Rais Donald Trump analenga kuwafurusha mamilioni ya wahamiaji nchini Marekani kinyume cha sheria na serikali yake imetaka kuongezwa idadi ya wahamiaji haramu kuelekea katika nchi ya tatu ikiwa ni pamoja kuwatuma huko Sudan Kusini na nchini Eswatini zamani Swaziland wahalifu waliopatikana na hatia.  

Uganda, mshirika wa Marekani  mashariki mwa Afrika pia imetoa hifadhi kwa wakimbizi karibu milioni mbili, wengi wao wakiwa wanatoka katika nchi za kanda hiyo kama  Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudan Kusini na Sudan.