Mrengo wa upinzani Somalia wafikia makubaliano na serikali kuhusu uchaguzi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i130036-mrengo_wa_upinzani_somalia_wafikia_makubaliano_na_serikali_kuhusu_uchaguzi
Mrengo uliojitenga na muungano mkuu wa upinzani nchini Somalia wa Salvation Forum umetia saini makubaliano ya uchaguzi na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na hivyo kutoa pigo kubwa kwa harakati kuu ya upinzani nchini humo.
(last modified 2025-08-27T02:28:35+00:00 )
Aug 27, 2025 02:28 UTC
  • Mrengo wa upinzani Somalia wafikia makubaliano na serikali kuhusu uchaguzi

Mrengo uliojitenga na muungano mkuu wa upinzani nchini Somalia wa Salvation Forum umetia saini makubaliano ya uchaguzi na Rais Hassan Sheikh Mohamud wa Somalia, na hivyo kutoa pigo kubwa kwa harakati kuu ya upinzani nchini humo.

Mrengo huo ambao ulikuwa ukiwajumuisha Omar Abdirashid Ali Sharmake waziri mkuu wa zamani wa Somalia, maspika wa bunge wa zamani Mohamed Mursal na Sharif Hassan Sheikh Adan, na mwanadilpmasia mkongwe Fahir Mohamud Gelle umejitenga na muungano mkuu wa upinzani wa Salvation Forum.  

Pande mbili zimesema katika taarifa ya pamoja iliyotolewa baada ya duru kadhaa za mazungumzo huko Mogadishu kwamba wamekubaliana na kuangalia upya mfumo wa uchaguzi ambao ungeiwkea nchi katika mfumo wa mtu mmoja, kura moja. 

Kwa mujibu wa makubaliano hayo, wabunge wa Shirikisho watachaguliwa kwa kura za wananchi, na mkabala wake watamchagua rais; hatua ambayo inaashiria kuachana kwa kiwango fulani na  mtindo wa uchaguzi usio wa moja kwa moja wa Somalia, ambapo wazee wa koo kwa kawaida huwachagua wabunge ambao baadaye hupiga kura kumchagua mkuu wa nchi.