EU kuiwekea vikwazo zaidi Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1309-eu_kuiwekea_vikwazo_zaidi_burundi
Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa uko tayari kuiwekea vikwazo zaidi nchi ya Burundi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 15, 2016 11:45 UTC
  • Bendera za EU
    Bendera za EU

Umoja wa Ulaya umetangaza kuwa uko tayari kuiwekea vikwazo zaidi nchi ya Burundi.

Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi za Umoja wa Ulaya wamesema leo kuwa wako tayari kutekeleza vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya Burundi. Uamuzi huo umechukuliwa baada ya kushindwa mazungumzo ya kukomesha mgogoro wa kisiasa wa Burundi ambao umesababisha mauaji ya watu zaidi ya 400.

Taarifa iliyotolewa na Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Ulaya mjini Brussels imesema kuwa umoja huo uko tayari kuchukua hatua za kukabiliana na watu wanaohusika na harakati za ukatili, ukandamizaji na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu.

Mwaka jana Umoja wa Ulaya ulianza kutekeleza baadhi ya vikwazo dhidi ya Burundi ikiwa ni pamoja na kuwapiga marufuku ya kufanya safari katika nchi za Ulaya maafisa wanne wa serikali ya Bujumbura walio karibu na Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo. Waafisa hao walituhumiwa kutumia vibaya madaraka yao katika mapigano ya ndani nchini Burundi.