Nigeria yatahadharisha kuhusu kuzidi kupenya kundi la Boko Haram barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1324-nigeria_yatahadharisha_kuhusu_kuzidi_kupenya_kundi_la_boko_haram_barani_afrika
Mkuu wa Kituo cha Upashaji Habari cha Taifa cha Nigeria ametahadharisha kuhusu hatari ya kuzidi kujitanua kundi la Boko Haram barani Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 15, 2016 21:37 UTC
  • Nigeria yatahadharisha kuhusu kuzidi kupenya kundi la Boko Haram barani Afrika

Mkuu wa Kituo cha Upashaji Habari cha Taifa cha Nigeria ametahadharisha kuhusu hatari ya kuzidi kujitanua kundi la Boko Haram barani Afrika.

Mkuu wa Kituo cha Upashaji Habari cha Taifa cha Nigeria amesema kuwa, hali ya mambo katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria hususan mji wa Maiduguri ambao ni makao makuu ya jimbo la Borno ni ya hatari sana.

Romery ametahadharisha kuwa kuenea harakati za kundi la Boko Haram barani Afrika ni hatari sana na kwamba iwapo wakuu wa nchi za Afrika hawatazingatia suala hilo, linaweza kuwa na athari mbaya na hatari sana kwa nchi mbalimbali.

Hadi kufikia sasa watu zaidi ya milioni mbili wamelazimika kuyahama makazi yao na kuwa wakimbizi katika nchi jirani tangu kuanza mapigano na mashambulizi ya Boko Haram huko Nigeria. Aidha watu zaidi ya elfu 13 wamepoteza maisha yao katika hujuma na jinai mbalimbali zinazofanywa na Boko Haram tangu mwaka 2010 hadi sasa. Wengi wa watu hao wamepoteza maisha katika mwaka mmoja uliopita.