Wanajeshi 12 wa Angola wauawa na waasi wa Cabinda
Waasi wa kundi la FLEC linalopigania kujitenga eneo la Cabinda huko Angola wamedai kuwa wameua wanajeshi wa serikali wasiopungua 12 katika eneo tajiri kwa mafuta kusini mwa nchi hiyo.
Kundi hilo kwa jina la Harakati ya Ukombozi wa Eneo la Cabinda wamebainisha kupitia taarifa waliyoitoa jana kuwa wapiganaji wa kundi hilo Jumapili iliyopita walitekeleza shambulio la kuvizia dhidi ya vikosi vya jeshi la Kongo kaskazini mwa eneo la Buco-Zau karibu na mpaka na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuua wanajeshi wasiopungua 12 na kuwajeruhi wengine kadhaa.
Waasi wa FLEC wamesema kuwa hadi sasa wameshawaua wanajeshi wa serikali wasiopungua 50 tangu kuanza mapigano baina yao na serikali ya Luanda. Hii ni katika hali ambayo serikali ya Angola hadi sasa haijatoa jibu lolote kuhusu madai hayo ya waasi wa Cabinda. Waasi hao wanaopigania kujitenga eneo la Cabinda huko Angola wamezidisha mashambulizi na hujuma za uharibifu tangu kuaga dunia mwezi Juni uliopita kiongozi wao mzee Nzita Tiago aliyekuwa na umri wa miaka 88.