Maandamano yapigwa marufuku Harare mji mkuu wa Zimbabwe
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i15244-maandamano_yapigwa_marufuku_harare_mji_mkuu_wa_zimbabwe
Duru za habari kutoka Zimbabwe zimearifu kuhusu kupigwa marufu kufanyika maandamano ya aina yoyote dhidi ya serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Sep 13, 2016 09:17 UTC
  • Maandamano yapigwa marufuku Harare mji mkuu wa Zimbabwe

Duru za habari kutoka Zimbabwe zimearifu kuhusu kupigwa marufu kufanyika maandamano ya aina yoyote dhidi ya serikali katika mji mkuu wa nchi hiyo Harare.

Duru rasmi huko Harare zimearifu kuwa polisi ya Zimbabwe imepiga marufuku kufanyika maandamano ya wapinzani dhidi ya serikali kwa muda wa mwezi mmoja katika mji mkuu huo. 

Douglas Mwonzora Katibu Mkuu wa Chama cha Mabadiliko ya Kidemokrasia ambacho ni chama kikuu cha upinzani huko Zimbabwe jana aliwatolea mwito wananchi kufanya maandamano ya nchi nzima dhidi ya serikali. 

Douglas Mwonzora Katibu Mkuu wa chama cha MDC 

Vyama vya upinzani vinavyoipinga serikali ya Rais Robert Mugabe vilikuwa vimewataka wananchi kufanya maandamano ya nchi nzima Jumamosi ijayo ili kuweza kufanikisha matakwa yao kuhusu kufanyika marekebisho katika suala la uchaguzi. Vyama hivyo vya upinzani vinataka uchaguzi mkuu wa mwaka 2018 uwe huru na wa haki. Upinzani na malalamiko yamezidi kuongezeka huko Zimbabwe tangu Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo aliye na umri wa miaka 92 atangaze nia yake ya kugombea tena kiti cha urais.