Mbio za kumrithi Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU zashika kasi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i17446-mbio_za_kumrithi_mwenyekiti_wa_kamisheni_ya_au_zashika_kasi
Kinyang'anyiro cha kuwania uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kimeendelea kupamba moto huku Chad ikimteua Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuwania nafasi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 15, 2016 08:22 UTC
  • Mbio za kumrithi Mwenyekiti wa Kamisheni ya AU zashika kasi

Kinyang'anyiro cha kuwania uenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kimeendelea kupamba moto huku Chad ikimteua Moussa Faki Mahamat, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuwania nafasi hiyo.

Mahamat atachuana na mawaziri wenzake Balozi Amina Mohammed wa Kenya, Agapito Mba Mokuy wa Equatorial Guinea, Pelonomi Venson-Moitoi wa Botswana pamoja na Abdoulaye Bathily raia wa Senegal ambaye kwa sasa ni mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika eneo la kati kati mwa Afrika.

Balozi Amina Mohammed, Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya

Mwenyekti mpya wa Kamisheni ya AU alikosa kupatikana katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika mjini Kigali, Rwanda mwezi Julai mwaka huu. Baada ya duru saba za upigaji kura, hakuna yeyote kati ya wagombeaji watatu aliyepata thuluthi tatu ya kura zilizohitajika kumpata mshindi.

Kiti hicho kimebaki wazi baada ya kumalizika muda wa mwenyekiti wa sasa, Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika Kusini ambaye aliteuliwa mwaka 2012, lakini hakuwania tena muhula wa pili wa miaka minne.

Uchaguzi huo unatazamiwa kufanyika Januari mwaka ujao 2017 mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.