Tahadhari kuhusu hali mabaya ya watu wa Ghaza
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1750-tahadhari_kuhusu_hali_mabaya_ya_watu_wa_ghaza
Harakati za Kiislamu na kitaifa za Palestina zimetahadharidha kuhusu hali mbaya ya watu wa eneo la Ukanda wa Gaza kutokana na mzingiro wa kidhalimu wa utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2016 00:09 UTC
  • Tahadhari kuhusu hali mabaya ya watu wa Ghaza

Harakati za Kiislamu na kitaifa za Palestina zimetahadharidha kuhusu hali mbaya ya watu wa eneo la Ukanda wa Gaza kutokana na mzingiro wa kidhalimu wa utawala haramu wa Israel dhidi ya eneo hilo.

Harakati za kupigania uhuru wa Palestina za Hamas, Jihad Islami, Harakati ya Wananchi ya Ukombozi wa Palestina, Harakati ya Kidemokrasia na makundi mengine yametoa taarifa yakisema kuwa, hali mbaya ya watu wa Gaza ni matokeo ya kuendelea mzingiro wa Israel dhidi ya watu wa eneo hilo, migawanyiko na hitilafu za ndani na kwamba mzingiro huo umezidisha umaskini, ukosefu wa ajira na mgogoro mkubwa.

Tamwimu zilizotolewa la shirika la Haki za Binadamu la Ulaya lenye makao yake huko Geneva, zinaonesha kuwa asilimia 40 ya wakazi wa Ukanda wa Gaza huko Palestina wanaishi katika umaskini uliopindukia na kwamba asilimia 80 miongoni mwao wanahitaji msaada wa chakula.

Mzingiro kamili wa eneo la Gaza ambao ulianzishwa na utawala ghasibu wa Israel mwaka 2007 umesababisha maafa makubwa kwa wakazi wa eneo hilo na kuwafanya wakose mahitaji ya kimsingi ya maisha kama chakula, dawa na kadhalika.