Wapinzani Niger wakataa matokeo ya awali ya uchaguzi
(last modified Wed, 24 Feb 2016 08:13:21 GMT )
Feb 24, 2016 08:13 UTC
  • Wapinzani Niger wakataa matokeo ya awali ya uchaguzi

Vyama vya upinzani Niger vimepinga matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais ambayo yalionyesha rais wa sasa Mahammadou Issofou akiongoza.

Matokeo ya awali ya maeneo 20 kati ya 308 yalionyesha kuwa Issofou alipata asilimia 40.18 ya kura zote, ikiwa ni pointi 10 mbele ya mpinzani wake wa karibu.

"Matokeo haya ni kinyume kabisa cha kile kilichodhihirika katika masanduku ya kupigia kura," alisema Ahmadou Boubacar Cisse mgombea urais na msemaji wa muungano wa upinzani.

Kumekuwepo na malalamiko ya wananchi kuhusu uendeshaji mbovu wa uchaguzi wa Rais uliofanyika siku ya Jumatatu nchini humo. Wapinzani wanasema kuwa tume ya uchaguzi ya nchi hiyo imevuruga kwa makusudi uchaguzi huo kwa maslahi ya rais aliyeko madarakani. Rais Mahamadou Issoufou amegombea kwa mara ya pili katika uchaguzi huo.

Tags