Zimbabwe yakataa wito wa kukubali ushoga na ndoa za jinsia moja
(last modified Tue, 08 Nov 2016 07:25:39 GMT )
Nov 08, 2016 07:25 UTC
  • Zimbabwe yakataa wito wa kukubali ushoga na ndoa za jinsia moja

Serikali ya Zimbabwe imesema katu haitokubali wito wa Umoja wa Mataifa wa kukubali ushoga na ndoa za jinsia moja katika nchi hiyo ya Kiafrika.

Emmerson Mnangagwa, Makamu wa Rais wa nchi hiyo amenukuliwa na gazeti la serikali la Herald akisema kuwa, Zimbabwe iko tayari kukubali mapendekezo mengine yote 142 ya UN ambayo yanaendana na katiba ya nchi, lakini suala la ushoga halitaruhusiwa nchini humo.

Emmerson Mnangagwa, Makamu wa Rais wa Zimbabwe

Mnangagwa ameliambia Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa kuwa, "Kuna baadhi ya nchi za Magharibi zinatushinikiza tukubali mahusiano ya jinsia moja lakini hilo haliwezekani kwa kuwa ni kinyume cha sheria katika nchi yetu."

Mwaka jana Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe alikiambia kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuwa, nchi yake kamwe haiwezi kuruhusu ushoga licha ya mashinikizo kutoka nchi za Magharibi na kusisitiza kuwa, haki za mashoga sio haki za binadamu kwa kuwa zinakinzana na mila, utamaduni, desturi na thamani za ubinadamu.

Maanamano dhidi ya ushoga nchini Mexico miezi miwili iliyopita

Nchi nyingi za Afrika zinatambua maingiliano ya kingono kati ya watu wenye jinsia moja kuwa ni kosa la jinai.

Katika miaka ya hivi karibuni, nchi kama Senegal, Burundi na Sudan Kusini zilipasisha sheria zinazotambua maingiliano kama hayo kuwa ni kosa la jinai huku Uganda, Nigeria na Liberia zikiwa mbioni kupasisha sheria zinazozidisha adhabu kwa wale wanaofanya vitendo hivyo vichafu.

Tags