Al Shabab yashambulia tena ikulu ya Rais Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i1945-al_shabab_yashambulia_tena_ikulu_ya_rais_somalia
Kundi la kigaidi la al Shabab limeshambulia ikulu ya Rais wa Somalia na kuua watu kadhaa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 25, 2016 22:32 UTC
  • Al Shabab yashambulia tena ikulu ya Rais Somalia

Kundi la kigaidi la al Shabab limeshambulia ikulu ya Rais wa Somalia na kuua watu kadhaa.

Ripoti zinasema wapiganaji wa kundi hilo la kigaidi jana walishambulia kwa mizinga ikulu ya Rais wa Somalia mjini Mogadishu na kuua watu wasiopungua 4 na kujeruhi wengine 8.

Msemaji wa kundi la al Shabab, Abdul Aziz Abu Mus'ab amethibisha kwamba, kundi hilo ndilo lililoshambulia ikulu ya Rais mjini Mogadishu.

Shambulizi la jana la al Shabab dhidi ya ikulu ya Rais wa Somalia limefanyika baada ya Rais wa nchi hiyo kuweka wazi kuwa askari baina ya 180 hadi mia mbili wa Kenya ambao ni sehemu ya kikosi cha askari wa Afrika cha kulinda amani nchini humo waliuawa katika shambulio la kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab dhidi ya kambi ya El-Adde mwezi uliopita.

Hadi sasa jeshi la Kenya halijatoa idadi rasmi ya wanajeshi wake waliouawa katika hujuma hiyo.