Libya kustafidi na uzoefu wa kiusalama wa Russia katika kupambana na ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i20440-libya_kustafidi_na_uzoefu_wa_kiusalama_wa_russia_katika_kupambana_na_ugaidi
Kamanda Mkuu wa vikosi vya Libya mashariki mwa nchi hiyo ametaka kutumiwa uzoefu wa kiusalama wa Russia katika mapambano dhidi ya ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 29, 2016 23:19 UTC
  • Libya kustafidi na uzoefu wa kiusalama wa Russia katika kupambana na ugaidi

Kamanda Mkuu wa vikosi vya Libya mashariki mwa nchi hiyo ametaka kutumiwa uzoefu wa kiusalama wa Russia katika mapambano dhidi ya ugaidi.

Jenerali Khalifa Haftar Kamanda Mkuu wa vikosi vya Libya mashariki mwa nchi hiyo ambaye yuko ziarani nchini Russia, amesema jana katika mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo kuwa anataraji kuwa magaidi wataangamizwa huko Libya kwa msaada wa Russia.

Jenerali Khalifa Haftar Kamanda Mkuu wa vikosi vya Libya mashariki mwa nchi

Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amebainisha kuwa Moscow inatambua nafasi ya jeshi la LIbya katika kulinda kujitawala na umoja wa ardhi ya nch hiyo kuwa ni ya thamani na kwamba itaendeleza juhudi zake ili kufanikisha mapatano ya kitaifa huko Libya kwa mujibu wa njia za utatuzi zilizopendekezwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Hii ni ziara ya pili ya Jenerali Khalifa Haftar  huko Russia katika muda wa mwezi mmoja; ambapo kamanda huyo wa jeshi amekutana na kufanya mazungumzo mjini Moscow na Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia.  Libya ilikumbwa na hujuma za magaidi na khususan kutoka kundi la kitakfiri la Daesh baada ya nchi hiyo kuupindua utawala wa kidikteta wa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.