Kongamano la Kimataifa la Amani na Usalama Afrika laanza Dakar
Kongamano la Tatu la Kimataifa Kuhusu Amani na Usalama Barani Afrika limenza leo mjini Dakar huko Senegal.
Kongamano hilo ambalo linafanyika kwa anwani ya Afrika Mkabala wa Changamoto za Kiusalama na Ushirikiano kwa Ajili ya Kupata Njia za Utatuzi" litaendelea kwa kipindi cha siku tatu.
Ajenda kuu ya Kongamano la Kimataifa la Usalama na Amani Barani Afrika ni kutafuta mzizi na chanzo cha matatizo ya kiusalama barani Afrika, kubadilishana habari za kiupelelezi na biashara, kukabiliana na changamoto zinazotishia usalama, kuzuia na kupambana na ugaidi, misimamo mikali na ukatili.
Marais, mawaziri, maafisa wa jeshi na wanadiplomasia wa nchi kadhaa za Afrika wanashiriki katika kongamano hilo wakiwemo Marais Muhammadu Buhari wa Nigeria, Salva Kiir wa Sudan Kusini, Ibrahim Boubakar Keita Mali na mwenyeji wao Macky Sall wa Senegal.
Nchi kadhaa za Afrika kama Burundi, Sudan Kusini, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Afrika ya Kati zinasumbuliwa na migogoro ya muda mrefu ya usalama.