Mgombea wa urais Niger ambaye yuko jela kuwania duru ya pili
(last modified Sun, 28 Feb 2016 07:56:33 GMT )
Feb 28, 2016 07:56 UTC
  • Mgombea wa urais Niger ambaye yuko jela kuwania duru ya pili

Rais wa sasa wa Niger Mahamadou Issoufou anayewania kuongoza kwa muhula wa pili atachuana na mpinzani wake wa karibu Hama Amadou, ambaye yuko kizuizini katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Machi 20 mwaka huu.

Kwa mujibu wa Tume ya Uchaguzi ya Niger, Rais Issoufou amepata asilimia 48.4 ya kura zilizopigwa katika uchaguzi wa Februari 21 na hivyo kushindwa kupata zaidi ya asilimia 50 ya kura hizo ili atangazwe mshindi. Amadou aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Niger na ambaye kwa sasa anashikiliwa na vyombo vya usalama kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya magendo ya watoto, alitangazwa kupata asilimia 17.8 ya kura. Mwanasiasa huyo ambaye alikuwa amekimbilia Ufaransa, alirejea nchini humo Novemba 14 mwaka uliopita. Mara tu baada ya kurejea vyombo vya usalama vilimtia mbaroni. Pamoja na kuendelea kushikiliwa korokoroni, Mahakama ya Katiba ilimuidhinisha kuwa miongoni mwa wagombea wa kiti cha urais.

Tags