Idadi ya walioaga dunia katika mlipuko Mogasdishu yafikia watu 35
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21220-idadi_ya_walioaga_dunia_katika_mlipuko_mogasdishu_yafikia_watu_35
Shambulio la bomu lililotekelezwa katika lango la kuingilia katika bandari kubwa zaidi ya Somalia huko Mogadishu, limeua watu 35 hadi sasa. Hayo ni kwa mujibu wa polisi ya Somalia.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 11, 2016 11:07 UTC
  • Idadi ya walioaga dunia katika mlipuko Mogasdishu yafikia watu 35

Shambulio la bomu lililotekelezwa katika lango la kuingilia katika bandari kubwa zaidi ya Somalia huko Mogadishu, limeua watu 35 hadi sasa. Hayo ni kwa mujibu wa polisi ya Somalia.

Mlipuko huo umetokea leo Jumapili katika bandari mashughuli ya Mogadishu baada ya mada za milipuko zilizokuwa zimetegwa ndani ya gari kulipuliwa na dereva mwenye gari. Maafisa wa huduma za dharura wameeleza kuwa watu wengine zaidi ya 50 wamejeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi. Kundi la kigaidi la al Shabab limedai kuhusika na shambulio hilo la leo huko katika bandari ya Mogadishu.

Majeruhi wakiondolewa mahali palipojiri shambulio huko Mogadishu 

Kundi la al Shabab jana pia lilifanya shambulio jingine la kulipua bomu karibu na mji mkuu Mogadishu na kusababisha vifo vya watu wawili. Kundi hilo lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida limekuwa likifanya oparesheni za kigaidi katika nchi hiyo maskini ya Kiafrika tangu mwaka 2006.