Uganda yaimarisha hatua za usalama kabla ya maandamano ya wapinzani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2152-uganda_yaimarisha_hatua_za_usalama_kabla_ya_maandamano_ya_wapinzani
Serikali ya Uganda imechukua hatua kali za usalama kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanywa leo na kambi ya upinzani nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 29, 2016 04:32 UTC
  • Uganda yaimarisha hatua za usalama kabla ya maandamano ya wapinzani

Serikali ya Uganda imechukua hatua kali za usalama kabla ya maandamano yaliyopangwa kufanywa leo na kambi ya upinzani nchini humo.

Ripoti zinasema vyombo vya usalama vya Uganda vimeimarisha ulinzi na hatua kali za usalama kote nchini kwa ajili ya kukabiliana na maandamano ya kambi ya upinzani yaliyoapngwa kufanyika hii leo.

Wapinzani wa Uganda wanalalamikia matokeo ya uchaguzi wa rais uliofanyika nchini humo Februari 18 ambapo kiongozi mkongwe wa nchi hiyo, Yoweri Museveni alitangazwa mshindi.

Polisi na jeshi la Uganda limetahadharisha kuhusu hatua yoyote ya kuvuruga amani na usalama katika maandamano hayo ya leo. Msemaji wa polisi ya Uganda, Patrick Onyango amesema polisi wamesambazwa katika miji yote mikubwa ya nchi hiyo kwa ajili ya kulinda usalama. Onyango amewataka wananchi kususia maandamano hayo.

Rais Yoweri Museveni alishinda uchaguzi wa rais na kumpiku mpinzani wake mkubwa Daktari Kizza Besigye kwa kupata asilimia 60 ya kura. Besigye amepinga matokeo hayo na kusema kuwa yamechakachuliwa.