Wapinzani S/Kusini wakaribisha mazungumzo ya kitaifa
-
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini
Wapinzani wa serikali ya Sudan Kusini wameunga mkono kufanyika mazungumzo ya kitaifa nchini humo.
Wapinzani hao wa serikali ya Juba leo wameunga mkono ombi la Rais Salva Kiir wa nchi hiyo la kutaka kufanyika mazungumzo ya kitaifa ili kurejesha amani, hata hivyo wameondoa uwezekano wa Kiir kushiriki kwenye mazungumzo hayo.
Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini juzi alitoa mwito wa kuanza mazungumzo ya kitaifa kwa kuyashirikisha makundi yote ya nchi hiyo.
Sudan Kusini ilitumbukia katika mzozo wa ndani na mgogoro wa kisasa tangu mwaka 2013 uliotokana na mapigano kati ya wafuasi wa Rais Salva Kiir na aliyekuwa Makamu wake Riek Machar.
Hali hiyo ya machafuko iliandaa uwanja wa kufanyika vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia, ubakaji na uhalifu mwingine dhidi ya wanawake huko Sudan Kusini bila ya wahusika kufikishwa katika vyombo vya sheria.