Maandamano dhidi ya serikali ya Sudan yaongezeka
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i21739-maandamano_dhidi_ya_serikali_ya_sudan_yaongezeka
Maandamano dhidi ya serikali ya Sudan yameshadidi sambamba na mgomo wa nchi nzima.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 19, 2016 11:20 UTC
  • Maandamano dhidi ya serikali ya Sudan yaongezeka

Maandamano dhidi ya serikali ya Sudan yameshadidi sambamba na mgomo wa nchi nzima.

Maandamano hayo yanaongezeka sambamba na wito wa vyama vya upinzani wa mgomo wa nchi nzima leo na kesho Jumanne huku vyombo vya usalama vya nchi hiyo vikishadidisha utumiaji mabavu dhidi ya wapinzani.

Vyama vya upinzanui na asasi za kijamii zimewataka raia kujitokeza na kushiriki katika maandamano dhidi ya serikali na hivyo kuendeleza upinzani wao wa wazi dhidi ya sera za serikali ya Khartoum za kubana matumizi.

Waandamanaji wanaolalamikia sera za Rais al-Bashir

Miongoni mwa mambo yanayolalamikiwa na wananchi wa Sudan ni kupanda gharama za umeme na mafuta ya petroli, ongezeko la ukosefu wa ajira na hatua ya idara za kiuchumi ya kuchukua maamuzi yasiyo na upimaji wa kina sambamba na kupuuzwa matakwa ya wananchi.

Maandamano hayo dhidi ya serikali yanazidi kushika kasi katika hali ambayo, maelfu ya raia wa taifa hilo wamekuwa wakisisitiza juu ya kukomeshwa mpango wa kutekelezwa siasa za kubana matumizi sanjari na kufanyika marekebisho ya kiutawala. 

Asasi za kiraia nchini Sudan, zimesisitiza juu ya kuendeleza maandamano dhidi ya serikali kwa ajili ya kupinga siasa mbovu za serikali ya rais Omar Hassan al-Bashir likiwemo suala la kupandisha bei ya mafuta.