Boko Haram yatoa vitisho vipya dhidi ya serikali ya Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22534-boko_haram_yatoa_vitisho_vipya_dhidi_ya_serikali_ya_nigeria
Kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram ametoa vitisho vipya dhidi ya jeshi la Nigeria.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 01, 2017 03:03 UTC
  • Boko Haram yatoa vitisho vipya dhidi ya serikali ya Nigeria

Kiongozi wa kundi la kigaidi la Boko Haram ametoa vitisho vipya dhidi ya jeshi la Nigeria.

Katika ujumbe wake wa mkanda wa video uliosambazwa  jana, Abubakar Shekau amekanusha madai ya serikali ya Nigeria iliyosema kuwa, kundi hilo limesambaratika, na amewataka wafuasi na wapiganaji wa kundi hilo kuzidisha mashambulizi dhidi ya jeshi la nchi hiyo. 

Jeshi la Nigeria limedai zaidi ya mara tatu kwamba limemuua kiongozi wa kundi la Boko Haram, Abubakar Shekau.

Abubakar Shekau na wapiganaji wenzake

Siku chache zilizopita Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria alitangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa kuwatimua wapiganaji wa kundi la Boko Haram katika ngome yao ya mwisho huko kaskazini mashariki mwa Nigeria na kwamba magaidi hao hawatakuwa tena na maeneo ya kujificha.

Uasi na mashambulizi ya miaka 7 sasa ya kundi la kigaidi la Boko Haram yameua zaidi ya watu elfu 20 na kuwalazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi.