Al Shabab washambulia ofisi ya Umoja wa Mataifa Mogadishu
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22834-al_shabab_washambulia_ofisi_ya_umoja_wa_mataifa_mogadishu
Kundi la kigaidi la al Shabab limeshambulia ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 04, 2017 13:00 UTC
  • Al Shabab washambulia ofisi ya Umoja wa Mataifa Mogadishu

Kundi la kigaidi la al Shabab limeshambulia ofisi ya Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Nour Othman ambaye ni afisa wa polisi ya Somalia amesema kuwa, gari lililokuwa limetengwa mabomu limeripuka leo kandokando ya ofisi za Umoja wa Mataifa mjini Mogadishu na kuua walinzi wanne wa eneo hilo. 

Othman ameongeza kuwa, gari hilo limelipuliwa mbele ya jengo la ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) mjini Mogadishu.

Kundi la kigaidi la al Shabab lenye mfungamano la al Qaida limetangaza kuwa ndilo lililofanya shambulizi hilo ambapo pia limejeruhi watu wengine kadhaa.

Image Caption

Jumatatu iliyopita pia maafisa watatu wa polisi waliuawa baada ya gari lililokuwa limetegwa mabomu kuripuka kwenye kituo cha upekuzi karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mogadishu.

Mlipuko huo ulitokea wakati maafisa usalama walipokuwa wanapekua magari katika umbali wa mita mia chache kutoka kambi ya kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika AMISOM na karibu na uwanja wa ndege wa Aden Adde.