Ombi la kuongezwa wanajeshi mashariki mwa Kongo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2302-ombi_la_kuongezwa_wanajeshi_mashariki_mwa_kongo
Wakazi wa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameomba kuzidishwa idadi ya wanajeshi katika eneo hilo ili kuwalinda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 02, 2016 10:44 UTC
  • Ombi la kuongezwa wanajeshi mashariki mwa Kongo

Wakazi wa eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameomba kuzidishwa idadi ya wanajeshi katika eneo hilo ili kuwalinda.

Wakazi wa eneo la Shabunda katika mkoa wa Kivu Kusini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wameiomba serikali ya nchi hiyo iongeze idadi ya wanajeshi katika eneo hilo. Drid Bambabwenge Msemaji wa wakazi wa eneo la Habunda ameeleza kusikitishwa na jinai zilizofanywa na wanajeshi kwa jina la "Raia Mutomboki" khususan katika barabara ya Burhale-Shabunda. Bambabwenge amewatuhumu wanamgambo wa "Raia Mutomboki" kwa kuwapora, kuwateka nyara na kufanya mashambulizi ya kuvizia dhidi ya raia. Hii ni katika hali ambayo eneo la mashariki mwa Kongo tangu miaka 20 iliyopita hadi sasa limeathiriwa na machafuko kufuatia kuwepo makundi ya waasi. Eneo hilo linaendelea kuathiriwa na machafuko kufuatia kushindwa jeshi la Kongo na wanajeshi wa kofia bluu wa Umoja wa Mataifa kuwaangamiza wanamgambo hao.