Watu wanne wauawa katika hujuma pacha mjini Mogadishu
Watu wasiopungua wanne wameuawa na wengine 17 kujeruhiwa katika mashambulizi pacha ya kigaidi yaliyoulenga mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Hujuma hizo zimejiri Jumamosi katika eneo la Banadir mjini Mogadishu ambapo maguruneti mawili zilitumika kushambulia mgahawa katika makutano ya Tarabuunka.
Mgahawa huo kwa kawaida hutumiwa sana na wanajeshi wa serikali. Msemaji wa Polisi ya Somalia katika eneo la Banaadir, Abdifatah Omar Halane amethiitisha kutokea hujuma hiyo na kusema idadi ya watu waliopoteza maisha, huenda ikaongezeka kwani baadhi ya majeruhi wako katika hali mahututi.
Maji wa Mogadishu umekuwa ukishuhudia mashambulizi ya mara kwa mara ya kigaidi na maafisa wa usalama wanasema kundi la kigaidi la Al Shabab lenye mfungamano na mtandao wa Al Qaeda ndilo linalofanya hujuma hizo zinazolenga maafisa wa serikali.
Hayo yanajiri wakati wabunge wa Somalia wanapanga kuteua maspika wa Mabunge mawili ya nchi hiyo na rais mpya baadaye mwezi huu wa Januari.