EAC yapata Katibu Mkuu mpya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i2326-eac_yapata_katibu_mkuu_mpya
Mwanadiplomasia wa Burundi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa nchi 5 za jumuiya hiyo mbali na kuidhinisha uanachama wa Sudan Kusini pia wamemteua Liberat Mfumukeko kuchukua nafasi ya Dkt. Richard Sezibera ambaye anamaliza muda wake.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 02, 2016 23:38 UTC
  • EAC yapata Katibu Mkuu mpya

Mwanadiplomasia wa Burundi ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki. Viongozi wa nchi 5 za jumuiya hiyo mbali na kuidhinisha uanachama wa Sudan Kusini pia wamemteua Liberat Mfumukeko kuchukua nafasi ya Dkt. Richard Sezibera ambaye anamaliza muda wake.

Liberat Mfumukeko ambaye ni mwanadiplomasia wa Burundi, atakuwa na jukumu la kuhakikisha mwanachama mpya wa EAC, yaani Sudan Kusini anafahamu vyema majukumu yake ndani ya muungano huo. Bw. Mfumukeko ambaye wakati mmoja alikuwa mshauri mkuu wa Rais Pierre Nkurunziza atakuwa na jukumu pia la kufuatilia mgogoro wa Burundi na jinsi ya kuutafutia ufumbuzi.

Marais wa nchi wanachama wa EAC pia wameidhinisha Rais John Pomb Magufuli wa Tanzania kuendelea kuwa mwenyekiti wa jumuiya hiyo kwa mwaka mwingine mmoja. Rais Magufuli amesema atashughulikia majipu makubwa na madogo kwenye jumuiya hiyo na kuyatumbua haraka.

Rais wa Uganda, Yoweri Museveni ameidhinishwa kuendelea kuwa msuluhishi mkuu wa kadhia ya Burundi.