UNSC yataka kukomeshwa migogoro magharibi mwa Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24031-unsc_yataka_kukomeshwa_migogoro_magharibi_mwa_afrika
Umoja wa Mataifa umetangza uungaji mkono wake kamili kwa juhudi za upatanishi na kuzuia migogoro na mivutano katika eneo la magharibi mwa Afrika.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jan 22, 2017 01:07 UTC
  • UNSC yataka kukomeshwa migogoro magharibi mwa Afrika

Umoja wa Mataifa umetangza uungaji mkono wake kamili kwa juhudi za upatanishi na kuzuia migogoro na mivutano katika eneo la magharibi mwa Afrika.

Taarifa iliotolewa leo na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa imeeleza wasiwasi wake kuhusu migogoro unayoshadidi katika eneo hilo, vitisho vya kigaidi, magendo ya dawa za kilevya na magendo ya wahajiri na binadamu wengine katika eneo la magharibi na Sahel barani Afrika, kuongezeka kwa harakati za maharamia katika Ghuba ya Guinea na hali mbaya ya kisiasa nchini Gambia, na imeitaja jamii ya kimataifa kufanya jitihada kubwa zaidi za kuunga mkono na kusaidia juhudi za upatanishi wa kimataifa kwa ajili ya kuboresha hali ya maeneo hayo.

Taarifa ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa pia imeeleza kufurahishwa na kuboreka kiasi hali ya kisiasa katika baadhi ya nchi za  Magharibi kwa Afrika kama vile kufanyika uchaguzi kwa uhuru na amani katika nchi za Cape Verde na Ghana na kuanza mazungumzo ya kisiasa katika nchi ya Gambia.

Wapatanishi wa Kiafrika katika mgogoro wa Gambia

Baraza la Usalama pia limepongea uamuzi uliochukuliwa na wanachama wake na vilevile Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika kuhusu mgogoro wa kisiasa nchini Gambia na kutoa wito wa kurejeshwa amani kamili katika nchi hiyo.

Baraza hilo limesema juhudi zinapaswa kudumishwa kwa ajili ya kuhamisha madaraka kwa amani nchini humo.