Abuja: Wanawake wa Boko Haram wanatumia vitoto vichanga katika mashambulizi ya kigaidi
(last modified Wed, 25 Jan 2017 03:00:12 GMT )
Jan 25, 2017 03:00 UTC
  • Abuja: Wanawake wa Boko Haram wanatumia vitoto vichanga katika mashambulizi ya kigaidi

Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa, baadhi ya wanawake wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram wanatumia watoto wachanga wanaonyonya kwa ajili ya kuwahadaa askari usalama na kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Maafisa wa serikali ya Nigeria wametahadharisha kuhusu mbinu hiyo ya Boko Haram ya kuwatumia watoto wachanga kwa ajili ya kupita katika vituo vya usalama na kufanya mashambulizi ya kigaidi.

Novemba mwaka jana wanachama wawili kike wa kundi hilo waliokuwa na watoto wanaonyonya waliingia katika soko lililokuwa limejaa watu katika mji wa Madagali jimboni Adamawa na kulipua mabomu ambayo yaliua raia wasiopungua 45. Hivi karibuni pia kundi hilo la kigaidi lilifanya shambulizi jingine kama hilo nchini Nigeria na kuua watu wasiopungua 25. 

Watoto wadogo pia wanatumwia na kundi la Boko Haram kujilipua kwa mabomu

Maelfu ya raia wasio na hatia wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi tangu kundi la Boko Haram lianze mashambulizi ya kigaidi na kujilipua kwa mabomu katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo mwaka 2009. 

   

Tags